array(0) { } Radio Maisha | Moto mkubwa ambao ulizuka katika kanisa la kihistoria jijini Paris, Notre Dame Cathedral hatimaye umethibitiwa kufuatia juhudi za zaidi ya wazima moto 500

Moto mkubwa ambao ulizuka katika kanisa la kihistoria jijini Paris, Notre Dame Cathedral hatimaye umethibitiwa kufuatia juhudi za zaidi ya wazima moto 500

Moto mkubwa ambao ulizuka katika kanisa la kihistoria jijini Paris, Notre Dame Cathedral hatimaye umethibitiwa kufuatia juhudi za zaidi ya wazima moto 500

Moto mkubwa ambao ulizuka katika kanisa la kihistoria jijini Paris, Notre Dame Cathedral  hatimaye umethibitiwa kufuatia juhudi za zaidi ya wazima moto 500 japo ikiwa ni baada ya kutekeleza uharibifu wa sehemu ya juu zaidi ya jumba hilo kwa kiingereza Spire. 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye amepiga kambi katika eneo la mkasa huo, amewapongeza wazima moto kwa kuthibiti moto huo dhidi ya kutekeleza uharibifu katika maeneo mengine ya jumba hilo kadhalika baadhi ya vifaa vya kihistoria vilivyohifadhiwa  huku akisema mpango wa kujenga upya sehemu zilizoharibika utaanza mara moja ikizingatiwa maana ya jengo hilo kwa kanisa katoliki na historia ya ufaransa kwa jumla.

Kanisa la Notre Dame limedumu kwa takriban miaka 850  tangu lilipoanza kujengwa mwaka  1160 na kukamilika katika karne ya 13. Tangu wakati huo kanisa limekuwa eneo la mtukio mengi ya kihistoria katika taifa la ufaransa kukiwamo kutawazwa kwa mfalme wa ufaransa Napoleon 1 mwaka 1804. Kanisa hilo limesalia kuwa kivutio kikubwa cha utalii na kutembelewa na zaidi ya watu milioni 13 kwa mwaka. Kadhalika katika maadhimisho ya wiki takatifu, kanisa hilo lilitarajiwa kutumika na waumini wa kanisa katoliki katika kuangazia historia ya kanisa katoliki hadi kufikia siku ya pasaka.

Rais wa Marekani ni miongoni mwa viongozi na watu tajika duniani ambao wamesikitishwa na mkasa huo nikinukuu. Nikinukuu So horrible to watch the massive fire at Notre Dame Cathedral in Paris. Perhaps flying water tankers could be used to put it out. Must act quickly!

Obama: Notre Dame is one of the world’s great treasures, and we’re thinking of the people of France in your time of grief. It’s in our nature to mourn when we see history lost – but it’s also in our nature to rebuild for tomorrow, as strong as we can.

“My thoughts are with the people of France tonight and with the emergency services who are fighting the terrible blaze at Notre-Dame cathedral.” – PM @Theresa_May