array(0) { } Radio Maisha | Kinara wa ODM Raila Odinga anatarajiwa kuwa mgeni mkuu katika Kongamano la Maseneta na Wawakilishi Wadi Kisumu

Kinara wa ODM Raila Odinga anatarajiwa kuwa mgeni mkuu katika Kongamano la Maseneta na Wawakilishi Wadi Kisumu

Kinara wa ODM Raila Odinga anatarajiwa kuwa mgeni mkuu katika Kongamano la Maseneta na Wawakilishi Wadi Kisumu

Kinara wa ODM Raila Odinga   anatarajiwa kuwa mgeni mkuu katika Kongamano la Maseneta na Wawakilishi Wadi linaloingia siku pili jijini Kisumu.  Raila atatoa mchango wake kuhusu hatua zilizopigwa na viongozi hao katika kufanikisha ugatuzi wakati ambapo mjadala mkali umeibuka kuhusu  umuhimu wa  kufanyika kwa makongamano hayo.

Hapo jana  kulishuhudiwa mvutano kati ya Kiongozi  wa Wachache katika Seneti James Orengo na wa wengi katika bunge hilo Kipchumba Murkomen baada ya Orengo kudai kuwa baadhi ya masuala yanayo jadiliwa katika makongamano hayo hayawajahi kutekelezwa hivyo kusalia eneo la mazungumzo tu.

 

Murkomen amepinga kauli hiyo ya Orengo akisema kuwa, Kongamano hio limeleta mabadiliko, akitumia mfano wa mwaka 2015 ambapo walitatua  matatizo ya Wawaikilishi Wadi hasa kuhakikisha wana akaunti tofauti isisyo chini ya serikali ya Kaunti.

Kadhalika, Murkomen amewashtumu magavana kwa madai ya kushirikiana na baadhi ya wabunge nchini, ili kuzipunguza fedha zinazotengewa mabunge ya kaunti. akisistiza hawatakubali fedha hizo kupunguzwa kwani wawakilishi wadi wamesaidia pakubwa katika kufanikisha ugatuzi. Vilevile Murkomen amesema wawakilishi wadi hawatanyanyaswa.

 

Vilevile suala kuu lililo ibuka katika kongamano hilo ni ukame kwenye kaunti kumi na tatu nchini. Suala ambalo Waziri wa Ugatuzi, Eugene Wamalwa,  alisisitiza kwamba kuna chakula cha kutosha ili kuwasaidia waathiriwa wa baa la njaa.  Aidha Wamalwa,  aliwasihi wawakilishi wadi kuweka mikakati mwafaka katika mabunge ya kaunti ,ili kuwasaidia waathiriwa wa kiangazi nchini.

 Kinyume na ilivyotarajiwa Rais Kenyataa hakudhuria Kongamano hilo hapo jana aidha alituma wawakilishi hatua ambayo imewakera baadhi ya wanaohuhudhuria. Hata hivyo kesho Naibu wake, William Ruto ameratibiwa kulifunga rasmi.