array(0) { } Radio Maisha | Atwoli anastahili kuweka wazi anochofahamu kuyahusu matamshi asema Khatib Mwashetani

Atwoli anastahili kuweka wazi anochofahamu kuyahusu matamshi asema Khatib Mwashetani

Atwoli anastahili kuweka wazi anochofahamu kuyahusu matamshi asema Khatib Mwashetani

Mbunge wa Lunga Lunga kwenye Kaunti ya Kwale Khatib Mwashetani, amekuwa wa hivi punde kuizungumzia kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU Francis,  kwamba Naibu wa Rais Daktari, William Ruto hatakuwa kwenye kinyang’anyiro kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Kulingana na Mwashetani, Atwoli anastahili kuweka wazi achanofahamu kuyahusu matamshi hayo,  ikizingatiwa kwamba hana mamlaka ya kusema ni nani anayestahili kuwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Haya yanajiri saa chache baada ya wabunge wa Chama cha ODM kutoa wito kwa Idara ya Upelelezi, DCI kuwachunguza viongozi wa Jubilee wanaojihusisha na kundi la TangaTanga,  ambalo limehusishwa na Naibu wa Rais William Ruto kwa madai ya kumhusisha  Atwoli na mauaji ya aliyekuwa Mbunge wa Kabete, George Muchai.

Wakiongozwa na Mbunge wa Saboti, Caleb Amisi, viongozi hao wamesema kauli ya Atwoli kwamba Naibu wa Rais hatakuwa debeni mwaka wa 2022 haikuwa na njama fiche jinsi wanavyodai wandani wa Ruto, kwamba huenda Atwoli anapanga kumuua.