array(0) { } Radio Maisha | Wakazi eneo la masinga Kaunti ya Machakos, wawashtaki maafisa wawili wa polisi

Wakazi eneo la masinga Kaunti ya Machakos, wawashtaki maafisa wawili wa polisi

Wakazi eneo la masinga Kaunti ya Machakos, wawashtaki maafisa wawili wa polisi

Wakazi wawili wa eneo la masinga Kaunti ya Machakos,  wamewashtaki maafisa wawili wa polisi wa kituo cha Kanyoonyoo  ambao waliwavamia na kuwajeruhi , baada ya wakazi hao kuwafumania wakiwa na msichana wa umri wa miaka 14 usiku , ambaye ni dadaye mwanaume mmoja kati ya waliojeruhiwa.

Benjamin Nzomo mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni kakaye msichana huyo,  alifahamishwa na jirani yake kuwa dadaye alikuwa na wanaume katika hoteli moja kwenye eneo hilo , kisha akaandamana na rafikiye kwa jina Daniel Mbaluka, na ndipo aliwapata maafisa hao wakiwa na dadaye.

Wawili hao wanasema walipojaribu kuwauliza maafisa hao walichokuwa wakifanya na mwanafunzi nyakati za usiku, wakawavamia kwa rungu kisha kuwazuilia katika Kituo cha Polisi cha Kanyoonyoo , huku wakilazimishwa kutia saini mkataba wa kutochukuliwa hatua.

Hata hivyo, kulingana na wakili atakayewawakilisha kwa jina Joel Mbaluka, wawili hao wameandikisha taarifa hii leo katika kituo cha polisi cha Masinga wakitaka haki itendeke.  Inaarifiwa kuwa msichana huyo  yatima, huuza mboga  wakati shule zimefungwa ili kumsaidia kakaye .

Aidha, kulingana na wakazi wa eneo hilo, maafisa hao, wanaoishi katika kijiji cha Musingi kaunti ya Kitui wamekuwa kero kwao kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi na wanaomba hatua za dharura zichukuliwe dhidi yao.