array(0) { } Radio Maisha | wabunge wa Chama cha ODM , sasa waitaka Idara ya Upelelezi, DCI kuwachunguza baadhi ya viongozi wa Jubilee

wabunge wa Chama cha ODM , sasa waitaka Idara ya Upelelezi, DCI kuwachunguza baadhi ya viongozi wa Jubilee

wabunge wa Chama cha ODM , sasa waitaka Idara ya Upelelezi, DCI kuwachunguza baadhi ya viongozi wa Jubilee

Baadhi ya wabunge wa Chama cha ODM , sasa wameitaka Idara ya Upelelezi, DCI kuwachunguza viongozi wa Jubilee wanaojihusisha na kundi la TangaTanga,  ambalo limehusishwa na Naibu wa Rais William Ruto kwa madai ya kumhusisha Katibu Mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi, COTU Francis Atwoli na mauaji ya aliyekuwa Mbunge wa Kabete, George Muchai.

Wakiongozwa na Mbunge wa Saboti, Caleb Amisi, viongozi hao wamesema kauli ya Atwoli kwamba Naibu wa Rais hatakuwa debeni mwaka wa 2022 haikuwa na njama fiche jinsi wanavyodai wandani wa Ruto kwamba huenda Atwoli anapanga kumuua.

Wakati uo huo, Amisi amesema ni sharti kundi la TangaTanga livunjiliwe mbali kwa kusababisha kupanda kwa joto la kisiasa nchini. Amesema iwapo kundi hilo lina ushahidi wowote kuhusu visa vya mauaji vinavyotekelezwa nchini, ni sharti waandikishe taarifa badala ya kusambaza uvumi.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya wandani wa Naibu wa Rais wakiongozwa na Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi, kumtaka Atwoli kutoa ufafanuzi kuhusu kauli yake.  Kwenye kikao na wanahabari mjini Eldoret,   Sudi ameyataja matamshi ya Atwoli kuwa yanayofichua njama ya baadhi ya wanasiasa dhidi ya Ruto.