array(0) { } Radio Maisha | Mwili wa mvulana wa miaka 9 wapatikana Chini ya Kitanda baada ya kutoweka katika hali ya kutatanisha.

Mwili wa mvulana wa miaka 9 wapatikana Chini ya Kitanda baada ya kutoweka katika hali ya kutatanisha.

Mwili wa mvulana wa miaka 9 wapatikana Chini ya Kitanda baada ya kutoweka katika hali ya kutatanisha.

Mwili wa mtoto mmoja wa miaka 9 aliyeripotiwa kutoweka siku ya Jumamosi umepatikana katika mtaa wa Kinamba mjini Naivasha.

Wakazi waliojawa na ghadhabu walimvamia na mshukiwa anayedaiwa kutekeleza  mauaji hayo na kumpiga hadi kumuua huku mama ya mshukiwa mwenyewe akijeruhiwa vibaya wakati wa tuko hilo.

Kwa mujibu wa walioshuhudia kisa hicho ni kwamba huenda mshukuwa huyo alimdhulumu mtoto huyo kingono kabla ya kumuua na kuuficha mwili wake chini ya kitanda.

OCPD wa eneo hilo John Kwasa amethibitisha kisa hicho na kusema  mwili ya mtoto huyo wa darasa la pili na ule wa mshukiwa imepelekwa katika hifadhi ya Hospitali ya kaunti ndogo ya Naivasha.