array(0) { } Radio Maisha | Hofu ya Madaktari ya usalama wa Madaktari yaongezeka baada ya wale wa Cuba kutekwa nyara

Hofu ya Madaktari ya usalama wa Madaktari yaongezeka baada ya wale wa Cuba kutekwa nyara

Madaktari kwenye Kaunti ya Kilifi sasa wanataka usalama kuimarishwa hata zaidi kwenye hospitali za humu nchini baada ya kutekwa nyara kwa madaktari wawili wa Cuba Ijumaa wiki iliyopita mjini Mandera.

Madaktari hao wamesema kwamba hospitali nyingi nchini hulindwa na walinzi wa kawaida ambao hawana uwezo wa kuwakabili magaidi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari, KMPDU tawi la Malindi, Evans Ogato aidha amesema wanapaswa kukabidhiwa silaha, akisema wahalifu huenda wanawalenga.

Ikumbukwe madaktari waliotekwa nyara bado hawajapatikana hadi kufikia sasa huku serikali ikisema kwamba wawili hao sharti wanusuriwe.

Madaktari hao ni Hazel Correa ambaye alikuwa ni daktari wa kawaida na Landy Roriguez ambaye alikuwa daktari wa upasuaji.

Wawili hao walitekwa nyara mapema Ijumaa wiki iliyopita na watu wanaoshukiwa kuwa wa kundi gaidi la Al-shabaab walipokuwa wakielekea kazini. Wakati wa makabilaino hayo afisa moja wa polisi ambaye alikuwa mlinzi wa madaktari hao aliuliwa kwa kupigwa risasi.

Hayo yanajiri huku serikari ikiwaagiza madaktari wengine waliokuwa wakihudumu kwenye Kuanti ya Garissa na Wajir kurejea Nairobi kutokana na sababu za kiusalama.