array(0) { } Radio Maisha | visa vya ajali za barabarani vyapungua Malindi kwa mujibu wa Idara ya trafiki.

visa vya ajali za barabarani vyapungua Malindi kwa mujibu wa Idara ya trafiki.

visa vya ajali za barabarani vyapungua Malindi kwa mujibu wa Idara ya trafiki.

Idara ya trafiki katika eneo la Malindi kwenye Kaunti ya Kilifi imesema visa vya ajali za barabarani sehemu hiyo vinaendelea kupungua kufuatia kuzingatiwa kwa sheria za trafiki.

George Naibei ambaye ni Kamanda wa Trafiki eneo hilo amesema idadi kubwa ya wahudumu wa bodaboda na madereva wa magari wanaendelea kuzingatia sheria, huku wanaovunja wakichukuliwa hatua kali.

Amesema kwamba asilimia 75 ya wahudumu wa bodaboda mjini Malindi wamezingatia sheria japo asilimia 75 ya wahudumu hao wa maeneo ya mashinani hawafuati sheria.

Amedokeza kwamba  wengi kwenye maeneo hayo ya mashinani wamekuwa wakiendeleza shughuli zao bila kuvaa helmeti, wengine wakikosa liseni mbali na kutokuwa na stakabadhi nyingine za kuwa barabarani.

Hata hivyo amesema kwamba idara yake itaendelea kuwakabili wahudumu hao.