array(0) { } Radio Maisha | Waumini wa madhehebu mbalimbali kote duniani yakiwamo Katoliki, Orthodox na ACK waadhimisha Jumapili ya Mitende, Palm Sunday

Waumini wa madhehebu mbalimbali kote duniani yakiwamo Katoliki, Orthodox na ACK waadhimisha Jumapili ya Mitende, Palm Sunday

Waumini wa madhehebu mbalimbali kote duniani yakiwamo Katoliki, Orthodox na ACK waadhimisha Jumapili ya Mitende, Palm Sunday

Waumini wa madhehebu mbalimbali kote duniani wamejumuika katika makanisa kwa maadhimisho ya Jumapili ya Mitende, Palm Sunday.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ameowaongoza maelfu ya waumini katika misa ambayo imefanyika kwenye makao makuu ya kanisa hilo, katika kanisa la St.Peters Square, jijini Vatican.

Awali akizungumza wakati wa misa ya hafla hiyo, Papa Francis amewahimiza waumini hao kudumisha mafunzo ya kidini kwa kuonesha upendo kwa watu wasiojiweza katika jamii.

Kadinali John Njue amewaongoza waumini wa kanisa hilo humu nchini katika maadhimisho hayo ambapo wamejumuika katika makanisa mbalimbali baada ya kutembea njiani wakibeba matawi ya mitende na kuimba.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, waumini hao walijumuika katika kanisa la Dayosisi ya Eldoret huku wa Trans Nzoia wakiadhimisha hafla yenyewe katika kanisa la Dayosisi ya Kitale.

Katika kaunti ya Nyerii, Askofu Antony Muheria aliongoza ibada hiyo katika kanisa la Dayosisi ya Nyeri Catheadral.

Mjini Kisumu, Askofu mkuu Philip Anyolo ameongoza shughuli hiyo ambapo amekariri umuhimu wa waumini kudumisha upendo na utangamano wa kitaifa.

Wakati wa maadhimisho hayo Kwenye kaunti ya Samburu, Askofu Virgilio Pante amewasihi wanasiasa hasa wanaoumini katika kanisa katoliki, kuwa mstari mbele katika kudumisha maadili ya kiimani. Amesema hali hiyo itasaidia pakubwa katika kukabili visa vya ufisadi.

kwenye Kaunti ya Mombasa, Waumini hao wamekongamana katika shule ya Msingi ya Star Of The Sea ambako walianza maombi ya uadhimishaji wa siku yenyewe wakiongozwa na Padri Raphael Kanga.

Ikumbukwe waumini wa kanisa katoliki huadhimisha siku hii ya Jumapili ya Mitende kila mwaka, kwa kufanya maandamano njiani huku wakiwa wamebeba matawi ya mti wa mtende yaani Palm Tree na kuimba nyimbo za ibada.

Desturi ya tukio hili kwa mujibu wa kanisa hilo, ni kuwa inatokana na siku ile ambapo Yesu wa Biblia aliingia mjini Yerusalemi kwenye msafara ulioibua taharuki katika kitabu cha Injili ya Mathayo 21 ; 9-10.

Madhehebu mengine yanayoadhimisha hafla hii ni likiwamo kanisa la Kiangilikana la ACK, Kanisa la Lutheran na Orthodox miongoni mwa mengine.