array(0) { } Radio Maisha | Katibu wa COTU Francis Atwoli ajipata Matatani kufuatia Matamshi yake kuhusu Naibu wa Rais

Katibu wa COTU Francis Atwoli ajipata Matatani kufuatia Matamshi yake kuhusu Naibu wa Rais

Katibu wa COTU Francis Atwoli ajipata Matatani kufuatia Matamshi yake kuhusu Naibu wa Rais

Hisia mbalimbali zinazidi kutolewa kufuatia matamshi ya Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi, COTU Francis Atwoli kwamba Naibu wa Rais William Ruto hatakuwa kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka wa 2022.

Mbunge maalumu David Ole Sankok, amemtaka Atwoli kutoa maelezo zaidi kuhusu kauli yake, akisema huenda ana njama fiche. Mbunge huyo hata hivyo amesema kwamba Chama cha Jubilee kitaafikiana ili kumpendekeza mtu mmoja kuwania kiti hicho hata kama hatakuwa Naibu wa Rais ili kuhakikisha kuna demokrasia chamani.

Ikumbukwe jana Seneta wa Kaunti ya Kericho, Aaron Cheruiyot vilevile alisema kwamba kauli ya Atwoli inapaswa kuchukuliwa kwa uzito. Seneta Cheruiyot anasema kwamba  Atwoli anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kufuatia matamshi yake.

Wakati uo huo, Sankok amependekeza kujiuzulu kwa Atwoli katika wadhifa wake iwapo anauheshimu demokrasia. Ameibua madai kwamba Atwoli amekuwa akitumia pesa ili kusalia kwenye wadhfa wa Katibu Mkuu katika COTU.