array(0) { } Radio Maisha | Waendeshaji pikipiki kwenye kaunti ya Isiolo wafunza sheria za trafiki

Waendeshaji pikipiki kwenye kaunti ya Isiolo wafunza sheria za trafiki

Waendeshaji pikipiki kwenye kaunti ya Isiolo wafunza sheria za trafiki

Wahudumu wa bodaboda wapatao 500 katika maeneo ya Bulapesa, Wabera na Burat kwenye kaunti ya Isiolo wamekamilisha mafunzo yao kuhusu sheria za trafiki kama njia moja ya kukabili ongezeko la visa vya ajali kwenye eneo hilo.

Akizungumza wakati wa kuwapokeza vyeti na leseni za kuhudumu barabarani, gavana Muhammed Kuti amewahimiza waendashaji bodaboda kwenye kaunti hiyo kuzingatia sheria za barabarani ili kupunguza ajali.

Kuti amewashauri waliokamilisha mafunzo yao kuwa kielelezo huku akidokeza kuwa serikali ya kaunti hiyo tayari imewasajili wengine 600 kwa lengo la kuwafadhili kwenye mafunzo yayo hayo.