array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta alaumiwa kwa kuchelewa kuwateua makamishna wapya wa Tume ya Ardhi, NLC.

Rais Kenyatta alaumiwa kwa kuchelewa kuwateua makamishna wapya wa Tume ya Ardhi, NLC.

Rais Kenyatta alaumiwa kwa kuchelewa kuwateua makamishna wapya wa Tume ya Ardhi, NLC.

 

Rais Uhuru Kenyatta amelaumiwa kwa kutoharakisha uteuzi wa makamishna wapya wa Tume ya Ardhi, NLC, hali ambayo imesababisha  kuongezeka kwa mzozo wa ardhi nchini.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Kenya Land Alliance, Odenda Lumumba amesema rais anakiuka katiba kwa kuchelewa kuwateua makamishna wengine baada ya muhula wa makamishna wa sasa kukamilika.

Kulingana na Lumumba, makamishna wa sasa hawawezi kusuluhisha mizozo ya arhdi, kupeana hati miliki wala kutunga sheria zozote kwani katiba haiwaruhusu baada ya muhula wa kuhudumu kukamilika.