array(0) { } Radio Maisha | Wazee wa Gare wa Mandera, kuelekea Somalia kuzungumza na wenzao kuhusu kutekwa nyara kwa madaktari wa Cuba

Wazee wa Gare wa Mandera, kuelekea Somalia kuzungumza na wenzao kuhusu kutekwa nyara kwa madaktari wa Cuba

Wazee wa Gare wa Mandera, kuelekea Somalia kuzungumza na wenzao kuhusu kutekwa nyara kwa madaktari wa Cuba

Wazee wa ukoo wa Garre wanatarajiwa kufanya mazungumzo na wenzao wa taifa la Somalia ili kuwanusuru madaktari wawili wa Cuba waliotekwa nyara mapema jana.

Gavana wa Kaunti ya Mandera, Ali Roba aidha amesema kwamba serikali yake itashirikiana na maafisa wa usalama katika harakati za kuwatafuta mateka hao.

Haya yanajiri huku Wizara ya Masuala ya Kigeni ikidokeza kwamba tayari serikali ya Cuba imejulishwa kuhusu kutekwa nyara kwa madaktari hao.

Waziri Monica Juma aidha amesema serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha kwamba madaktari hao ambao wanaaminika kutekwa nyara na Kundi gaidi la Alshabab, wananusuriwa.

Hata hivyo msemaji wa polisi, Charles Owino amesema kwamba tayari madaktari hao wamevuka mpaka hadi taifa jirani la Somalia.

Ikumbukwe vilevile Chama cha Madaktari, KMPDU kimelaani kitendo hicho huku kikitaka serikali kuwahakikishia wanachama wake usalama hasa wanaofanya kazi kwenye maeneo hatari.

Madaktari hao ni Hazel Korea ambaye alikuwa ni daktari wa kawaida na Landy Roriguez ambaye alikuwa daktari wa upasuaji.