array(0) { } Radio Maisha | Bensouda apokonywa viza na serikali ya Marekani

Bensouda apokonywa viza na serikali ya Marekani

Bensouda apokonywa viza na serikali ya Marekani

Serikali ya Marekani imempokonya viza Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya ICC, Fatou Bensouda kufuatia hatua yake ya kuchunguza mauaji kati ya Marekani na Afghanistan.

Katibu Mkuu wa Marekani, Mike Pompeo amesema Marekani iliamua kuwapokonya viza maafisa wote wa ICC kufuatia madai kwamba wanachunguza visa vya mauaji dhidi yake.

Pompeo amesema ni kinyume kwa Bensouda kuchunguza visa hivyo ilhali Marekani si mwanachama wa Mkataba wa Roma uliobuni Mahakama ya ICC.

 

Hata hivyo mahakama hiyo itaendeleza shughuli zake za kuchunguza visa vya mauaji kati ya Marekani na Afghanistan.

Katika taarifa iliyotumwa katika vyombo habari, Mkuu wa Mashtaka katika mahakama hiyo, Fatou Bensouda ataendelea na uchunguzi wake bila kuhofu lolote.

Majaji katika mahakama hiyo aidha wamesema zaidi ya stakabadhi 100 tayari zinafanyiwa ukaguzi kwenye uchunguzi ulionza mwaka wa 2017.