array(0) { } Radio Maisha | Mwili wa Daktari, Ali Hamisi Juma aliyefariki dunia akiwa nchini Cuba kuzikwa Ijumaa

Mwili wa Daktari, Ali Hamisi Juma aliyefariki dunia akiwa nchini Cuba kuzikwa Ijumaa

Mwili wa Daktari, Ali Hamisi Juma aliyefariki dunia akiwa nchini Cuba kuzikwa Ijumaa

Mwili wa Daktari, Ali Hamisi Juma aliyefariki dunia akiwa nchini Cuba unazikwa Ijumaa baada ya sala. Mwili huo umewasili nchini mapema leo kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mombasa. Familia ya marehemu ikiongozwa na Mbunge wa Likoni Mishi Mboko, imewaongoza waombolezaji wengine kuupokea mwili huo.

Mazishi yatafanyika baada ya mwili kufanyiwa upasuaji katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya Mombasa ili kubainisha kilichosababisha kifo chake.

Daktari Juma anasemekana kujiua kufuatia mafadhaiko aliyokuwa akiyapitia nchini Cuba hasa baada ya serikali kukataa ombi lake la kutaka kurejea nchini. Kisa hicho kimeibua mjadala mkali humu nchini, hasa kuhusu mazingira ya kufanyia kazi ya madaktari hao wa Kenya walioko Cuba na kiwango cha mshahara wanachopokea.

Hapo jana serikali iliahidi kuwa itawalipa marupurupu zaidi madakatri hao 50. Katibu wa Wizara ya Afya, Susan Mochache alisema madktari hao sasa watakuwa wakilipwa shilingi elfu mia moja arubaini na nne kila mwezi kinyume na shilingi elfu hamsini mia nane ambazo wamekuwa wakilipwa. Hatua hii inamaanisha kuwa kila daktari atalipwa shilingi laki nne kila mwezi, pamoja na mshahara ambao walikuwa wakilipwa nchini kabla ya kuelekea Cuba.