array(0) { } Radio Maisha | Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo

Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo

Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo

Watafiti nchini Uingereza wamebainisha kwamba raia mmoja wa taifa hilo aliyekuwa akiugua na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi, HIV hana tena virusi hivyo. Mgonjwa huyo ambaye pia amekuwa akiugua saratani amekuwa akifuatiliwa kwa kipindi cha miezi 18 sasa na kuabinika kwamba viini vinavyosababisha maradhi hayo havionekani tena katika mwili wake baada ya kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha hali hiyo kwa kuwekewa chembechembe zisizokuwa na maradhi.

 Watafiti hao wa  Chuo cha University College London, Imperial College London, na vyuo vikuu vya Cambridge na Oxford hata hivyo wamesema bado ni mapema kutangaza rasmi kuwa mgonjwa huyo amepona kabisa. Mwanamume huyo alibainika kuugua ugonjwa wa Ukimwi mwaka 2003.

Kisa kingine cha mgonjwa kuripotiwa kupona ugonjwa huo, ilikuwa miaka takriban kumi iliyopita ,ambapo mgonjwa aliyefanyiwa bone marrow transpant alipona kabisa.