array(0) { } Radio Maisha | Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi atangaza rasmi kuwa wazi wa viti vya ubunge vya maeneo hayo

Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi atangaza rasmi kuwa wazi wa viti vya ubunge vya maeneo hayo

Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi atangaza rasmi kuwa wazi wa viti vya ubunge vya maeneo hayo

Tume ya Uchaguzi IEBC imetangaza kuwa chaguzi ndogo za maeneo bunge ya Embakasi Kusini na Ugenya zitafanyika tarehe 5 mwezi Aprili, huku wanowania wakipewa hadi tarehe 21 mwezi huu kujisajili.

Hayo yanajiri baada ya Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi kutangaza rasmi kuwa wazi wa viti vya ubunge vya maeneo hayo baada ya Mahakama ya Juu kutupilia mbali ushindi wa wabunge hao na kutoa amri kwa Tume ya Uchaguzi, IEBC kurudia uchaguzi kwenye maeneo hayo.

Ushindi wa Mbunge wa Embakasi Kusini, Julius Mawathe ulitupiliwa mbali na Mahakama ya Juu huku Jaji Mkuu, David Maraga akisema matokeo yaliyotangazwa na IEBC hayakuonesha ushindi wa Mawathe.

Kesi hiyo iliwasilishwa na mpinzani wa Mawathe, Irshad Sumra aliyedai mashine za kuwatambua wapigakura za KIEMS zilifeli katika vituo vitatu vya kura.

Vilevile, mahakama hiyo ilitupilia mbali ushindi wa Chris Karani, Mbunge wa Ugenya.