array(0) { } Radio Maisha | Ekari 20 kati ya Ekari 26 inayomiliki Buatani ya Mama Ngina Drive jijini Mombasa inamilikiwa na watu binafsi kinuyume na sheria

Ekari 20 kati ya Ekari 26 inayomiliki Buatani ya Mama Ngina Drive jijini Mombasa inamilikiwa na watu binafsi kinuyume na sheria

Ekari 20 kati ya Ekari 26 inayomiliki Buatani ya Mama Ngina Drive jijini Mombasa inamilikiwa na watu binafsi kinuyume na sheria

Mabwenyenye wote walionyakua ardhi ya inayomiliki bustani ya Mama Ngina Drive wamepewa makataa ya siku tisini kurudisha ardhi hiyo.Makataa hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Tume ya itaifa ya Ardhi NLC, Mohamed Swazuri ambaye amezuru eneo hilo na baadhi ya makamishna wa ardhi wa Kaunti hiyo.

Kauli hiyo inajiri siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuiagiza NLC na Wizara ya Ardhi kuhakikisha vipande vyote vya ardhi ambavyo vimepakana na Bustani ya Mama Ngina Drive vilivyo nyakuliwa vimerudishiwa serikali kabla mwezi Juni mwaka huu.

Ekari 20 kati ya Ekari 26 inayomiliki Buatani ya Mama Ngina Drive jijini  Mombasa inamilikiwa na watu binafsi kinuyume na sheria

Ikumbukwe Swazuri alirejea kazini kufuatia agizo la mahakama baada ya kuhusishwa na ukiukaji wa sheria katika kuwafidia watu ambao ardhi zao zilitwaliwa kupisha ujenzi wa reli ya kisasa, SGR.

Aidha kurudi kwake ofisini kulipingwa na Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Hajji akitaka kesi iamuliwe kwanza.