array(0) { } Radio Maisha | Raia wa Uchina wazuiliwa kwa madai ya kupatikana na nyama ya mbwa na bidhaa za wanyamapori

Raia wa Uchina wazuiliwa kwa madai ya kupatikana na nyama ya mbwa na bidhaa za wanyamapori

Raia wa Uchina wazuiliwa kwa madai ya kupatikana na nyama ya mbwa na bidhaa za wanyamapori

Mahakama ya Milimani imewaruhusu polisi kuwazuilia raia watatu wa Uchina na Mkenya mmoja kwa kipindi cha siku tano kwa kupatikana na nyama inayokisiwa kuwa ya mbwa na bidhaa nyingine za wanyamapori eneo la Kilimani, Nairobi.

Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo ametoa uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka kusema haukuwa umekamilisha uchunguzi kuhusu bidhaa zilizokuwa zimenaswa, japo idara zinazohusika zinaendelea na uchunguzi zaidi. 

Mahakama aidha imeelezwa kuwa mmoja wa washtakiwa hajawakabidhi polisi paspoti yake ya usafiri, hali ambayo huenda ikamfanya kutoweka nchini huku mwingine akipatikana na viza ya usafir ambayo muda wake wa kutumiwa umekamilika.

Kabla ya mahakama kutoa uamuzi wa kuwazuilia, mawakili wa washtakiwa walitaka kuachiliwa huru kwa wateja wao kwa misingi kwamba hapakuwa na misingi thabiti ya kuwazuilia.