array(0) { } Radio Maisha | Gavana Sonko ajitenga na madai ya kuongoza kupitia vitisho

Gavana Sonko ajitenga na madai ya kuongoza kupitia vitisho

Gavana Sonko ajitenga na madai ya kuongoza kupitia vitisho

Gavana wa Nairobi, Mike Mbuvi Sonko ametetea uongozi wake wa jiji na kupuuzilia mbali madai ya kutumia vitisho dhidi ya mawaziri wake, hali iliyodaiwa kushinikiza kujiujulu kwa Waziri wa Elimu, Janet Muthoni Ouko.

Akimkosoa Muthoni kufuatia hatua yake ya kujiuzulu na kudai kufanya hivyo kufuatia vitisho kutoka kwa Gavana, Sonko amedai kwamba Janet amehusika katika ufujaji wa fedha hali ambayo imemlazimu kujiuzulu.

Sonko ameitaka idara ya upelelezi DCI na Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC kuanzisha uchunguzi dhidi ya Janet akidai kwamba amehusika katika ubadhirifu wa fedha za umma.

Kwenye mahojiano na Runinga na KTN  kwa njia ya simu baada ya Gavana Sonki kumstumu, Janet amesisitiza kuwa hajutii hatua yake ya kujiuzulu huku akimtaja Sonko kuwa kiongozi anayetumia propaganda kuwaharibia sifa viongonzi wenye mtazamo tofauti na wake.