array(0) { } Radio Maisha | Watu watano wa familia moja wafariki dunia kwenye mkasa wa moto Nyandarua

Watu watano wa familia moja wafariki dunia kwenye mkasa wa moto Nyandarua

Watu watano wa familia moja wafariki dunia kwenye mkasa wa moto Nyandarua

Huzuni imetanda kwenye kijiji cha Gita, Kipipiri Kaunti ya Nyandarua baada ya watu watano wa familia moja kuteketea kufuatia mkasa wa moto usiku wa kuamkia leo. Miongoni mwa waliofariki dunia ni mume na mkewe pamoja na wanao watatu wenye umri wa kati ya miezi mitatu na kumi na mitatu.

Mkuu wa Polisi wa Kipipiri, Charles Rotich amesema majirani walisikia mlipuko mkubwa katika nyumba ya mbao ya watu hao. Juhudi za wakazi kuukabili moto huo hazikufua dafu kufuatia upepo mkali uliokuwa ukivuma.

Mili imepelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya JM eneo la Ol Kalau huku uchunguzi kuhusu kisa hicho ukianzishwa.