array(0) { } Radio Maisha | Ali Bongo ametawala kuanzia mwaka wa 2009 baada ya kufariki kwa babaye Omar Bongo

Ali Bongo ametawala kuanzia mwaka wa 2009 baada ya kufariki kwa babaye Omar Bongo

Ali Bongo ametawala kuanzia mwaka wa 2009 baada ya kufariki kwa babaye Omar Bongo

Wananchi wa taifa la Gabon wako katika  njia panda wasijue la kufanya baada ya wanajeshi kupindua serikali wakidai ni njia moja wapo ya kurudisha demokrasia katika taifa hilo.

Wanajeshi hao walitangaza mapinduzi hayo katika kituo cha Redio cha Taifa saa kumi na moja saa za Kenya, wakiamrisha wanajeshi kudhibiti mbinu zote za usafiri na kushika doria katika uwanja wa ndege.

Wanajeshi hao wametaja kusikitishwa na hotuba ya mwaka mpya ya Rais Ali Bongo kuwa yu katika hali nzuri ya afya kuendelewa kutawala, hasa baada ya kujulikana wazi hali yake ya afya imedorora.

Ali Bongo ametawala kuanzia mwaka wa 2009 baada ya kufariki kwa babaye Omar Bongo. Aidha kwa miezi miwili amekuwa akitibiwa katika taifa la Morocco baada ya kuugua kiarusi yaani stroke.

Magari ya wanajeshi na wanajeshi waliojihami yameonekana katika Mji Mkuu wa Libreville.