array(0) { } Radio Maisha | Murathe asema yu huru kumsuta Ruto baada ya kujiuzulu

Murathe asema yu huru kumsuta Ruto baada ya kujiuzulu

Murathe asema yu huru kumsuta Ruto baada ya kujiuzulu

Aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Jubilee, David Murathe sasa amesema yu huru kuendeleza shutma dhidi ya Naibu wa Rais, William Ruto ambaye anapinga azma yake ya kuwania urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Murathe amemshtumu Ruto kwa madai ya kuhusika ufisadi akilitaja suala hilo kuwa mojawapo ya sababu zake kuu za kumpinga.

Murathe amedai kuwa kuna wanasiasa wengine ndani na nje ya  Chama cha Jubilee ambao pia wanampinga Ruto lakini wamekosa ujasiri wa kujitokeza wazi alivyofanya. Aidha amesema yu tayari kushirikiana na kiongozi yeyote anayempinga naibu huyo wa Rais.

Wakati uo huo amepinga madai kwamba alishinikizwa na kiongozi wa chama hicho, Uhuru Kenyatta kujiuzulu na kusema Uhuru hakuwa na ufahamu kuhusu mipango yake ya kujiuzulu. Aidha amesema kauli ambazo amekuwa akitoa dhidi ya Ruto ni zake binafsi wala hajashinikizwa na yeyote.  

Ikumbukwe Murathe alitangaza kwamba atawasilisha kesi katika Mahakama ya Juu kupinga azma ya Ruto kuwania urais akisema muda wake wa kuhudumu unakamilika sambamba na wa Rais Kenyatta na hafai kuendelea kuhudumu.