array(0) { } Radio Maisha | Azma ya Ruto kuwania urais yaendelea kupigwa vita

Azma ya Ruto kuwania urais yaendelea kupigwa vita

Azma ya Ruto kuwania urais yaendelea kupigwa vita

Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi, Beatrice Elachi amewakosoa wabunge wa eneo la Magharibi ya nchi wanaomuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto kwenye azma yake ya kuwania urais 2022.

Akizungumza eneo la Lugari, Elachi ambaye kwa muda mrefu amekuwa mfuasi wa Ruto amelitaka eneo la Magharibi kubadili mawazo na kuanza kumtambua Musalia Mudavadi ili kumwezesha kuchukua hatamu za uongozi wa taifa ifikapo mwaka  2022.

Hata hivyo, amemrai Mudavadi kufanya kazi kwa karibu na serikali ya ilioko ili kuongeza nafasi yake ya kuliongoza taifa hili.

Katika siku za hivi karibuni Ruto amekuwa akiandamwa kisiasa na viongozi wanaopinga azma yake ya kuwania urais huku Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Jubilee, David Murathe akiendeleza ukosoaji dhidi yake akisema hafai kuwania muhula mwingine wa uongozi kwani amehudumu sambamba na Rais Uhuru Kenyatta ambaye muda wake unakamilika.

Akihutubu wakati wa hafla ya mazishi ya nduguye Katibu Mkuu wa Jubilee, Raphalel Tuju, Murathe amesema atawasilisha kesi katika Mahakama ya Juu kwa lengo la kumzuia Ruto kuwania urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.