array(0) { } Radio Maisha | Polisi mmoja ajiua kwa kujipiga risasi Mombasa

Polisi mmoja ajiua kwa kujipiga risasi Mombasa

Polisi mmoja ajiua kwa kujipiga risasi Mombasa

Polisi kwenye Kaunti ya Mombasa wanakichunguza kisa ambapo afisa mmoja wa polisi amejiua kwa kujipiga risasi leo asubuhi katika Bandari ya Mombasa.

Afisa huyo kwa jina Charles Ndolo, aliyekuwa akihudumu katika Kituo cha Polisi cha Kipevu, anadaiwa kujipiga risasi akiwa chooni. Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Bandari ya Mombasa, Partrick Lobolia amethibitha kisa hicho. Afisa huyo ametumia bunduki aina ya AK 47 kujiua.

Mwili umepelekwa katika Chumba cha Kuhifadhi Maiti cha Hospitali ya Coast General.