array(0) { } Radio Maisha | Mume na mkewe wajeruhiana kwa visu Kitui

Mume na mkewe wajeruhiana kwa visu Kitui

Mume na mkewe wajeruhiana kwa visu Kitui

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 44 pamoja na mkewe mwenye umri wa miaka 30 wanaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Katulani Level 4, Kaunti ya  Kitui baada ya kujeruhiana kwa visu walipokuwa wakipigana kufuatia mzozo wa kinyumbani.

Kamanda wa Polisi kaunti hiyo, Benson Wasike, amesema wawili hao waliokolewa na maafisa wa polisi wakiwa wamezirai kufuatia kutokwa na damu nyingi na kupelekwa hospitalini.  

Mwanamke huyo kwa jina Maria Kyavati ana majeraha ya uso baada ya kisu kukwama karibu na jicho vilevile majeraha mengine mwilini huku mumewe  Kyavati Kioko akiwa na jeraha kubwa la kisu shingoni na katika sehemu za siri.  

Inaarifiwa wawili hao wamekuwa na mizozo ya mara kwa mara na wamekuwa wakisaidiwa na majirani vilevile wazee wa jamii kupata ushauri.