array(0) { } Radio Maisha | Waititu ampa likizo ya lazima Waziri wa Kilimo

Waititu ampa likizo ya lazima Waziri wa Kilimo

Waititu ampa likizo ya lazima Waziri wa Kilimo

Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu amempa likizo ya lazima Waziri wa Kilimo na Mauzo kwenye kaunti hiyo, John Ngigi.

Waititu amesema amechukua hatua hiyo kwa kuwa Ngigi amesalia kazini kwa muda mrefu bila kuchukua mapumziko kutokana na majukumu ya wadhifa wake. Waititu amemwagiza kuelekea kwa likizo ya siku thelathini kuanzia leo hii.

Ngigi ambaye ni nduguye Mbunge wa Gatungu Kusini, Moses Kuria ameagizwa kumkabidhi majukumu yake Waziri wa Mifugo. Anatarajiwa kurejea kazini Februari 14.