array(0) { } Radio Maisha | Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa KEBs, Charles Ongwae aachiliwa kwa dhamana

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa KEBs, Charles Ongwae aachiliwa kwa dhamana

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa KEBs, Charles Ongwae aachiliwa kwa dhamana

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa, KEBs Charles Ongwae ameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi laki tatu pesa taslimu ama bodi ya shilingi laki tano baada ya kukana mashtaka ya ufisadi yanayomkabili. Ongwae anatuhumiwa kuchangia kupotea kwa shilingi milioni 64.9 fedha za serikali baada ya kutoa agizo la kupunguzwa kwa kodi inayotozwa bidhaa zinazoingizwa nchini bila cheti muhimu kutoka taifa zinakotoka kutoka asilimia 15 hadi asilimi 0.5.

Amekana mashtaka dhidi yake mbele ya Hakimu, Kennedy Cheruiyot siku moja baada ya washukiwa wengine 11 kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zizo hizo. Inadaiwa mnamo mwezi Januari mwaka uliopita, Ongwae na washukiwa wengine wakiwamo Eric Chesire, Samuel Mburu, Hillary Kamau, Ibrahim Twahir na kampuni za Gendpie Enterprises, Rupai Trading Limited na Landmark Freight Services Limited walishirikiana kuipora serikali fedha hizo. 

Ongwae anakabiliwa na shtaka jingine la matumizi mabaya ya ofisi. Mahakama imeagiza kwamba  afike katika  Idara ya Upelelezi, DCI siku ya Jumatatu wiki ijayo kurekodi taarifa huku kesi dhidi yake ikitajwa Januari 14.