array(0) { } Radio Maisha | Uteuzi wa makamishna wapya wa NPSC waendelea

Uteuzi wa makamishna wapya wa NPSC waendelea

Uteuzi wa makamishna wapya wa NPSC waendelea

Watu walio na nia ya kuwania nyadhifa mbalimbali katika Tume ya Huduma za Polisi, NPSC wana hadi leo kuwasilisha maombi yao. Tayari nafasi ya Mwenyekiti na makamishna wa tume hiyo zimetangazwa kuwa wazi. Mwenyekiti wa kamati inayoongoza uteuzi wa maafisa hao, Stephen Kirogo amesema wanalenga kuwateua makamishna watatu kutoka kwa umma huku makamishna wengine wawili wakistahili kuwa maafisa wa polisi waliostaafu.

Majina ya watakaoteuliwa ili kufanyiwa mchujo yatachapishwa magazetini.  Aidha watakaoteuliwa watafahamishwa kuhusu stakabadhi wanazostahili kuwasilisha wakati wa mchujo. Uteuzi wa Mwenyekiti na makamishna hao unajiri kufuatia kukamilika kwa muda wa kuhudumu kwa miaka sita wa tume iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti, Johstone Kavuludi.

Wanakamati wengine wanaohusika katika uteuzi wa maafisa wapya wa NPSC ni Kennedy Kihara kutoka kwa ofisi ya Baraza la Mawaziri, Anne Amadi wa Idara ya Mahakama, Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC  Twalib Mbarak, Kagwiria Mbogori wa Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Kibinadam, Joyce Mwikali wa Tume ya Jinsia na Samson Kibii.