array(0) { } Radio Maisha | Wizara ya Leba kuanza mikutano ya kusuluhisha migomo ya walimu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wizara ya Leba kuanza mikutano ya kusuluhisha migomo ya walimu

Wizara ya Leba kuanza mikutano ya kusuluhisha migomo ya walimu

Kamati maalum iliyobuniwa na Waziri wa Leba itaaza rasmi mikutano na washikadau kadhaa katika sekta ya elimu Jumamosi kutafuta suluhu ya mgomo wa walimu unaotishia kuanza wiki ijayo.

Waziri wa Leba Ukur Yattani amesema kamati maalum iliyobuniwa kuongoza mazungumzo hayo itaongozwa na Charles Maranga. huku wanachama wengine wakiwa ni Moses Ombokh, Isaiah Kubai, Linus Kariuki, Albert Njeru,  Robert Muthanga na Benson Okwaro. Walter Kinjo anakamilisha taraifa hiyo.

Kamati hiyo tayari imekutana leo hii na kutoa ratiba kwa Tume ya Huduma za Walimu na Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT kufuatia mikutano ambayo imeratibiwa kuanza wiki ijayo.

Kamati hiyo kesho inatarajiwa kuzuru makao makuu ya KNUT jijini Niarobi ambapo inatarajiwa kufanya mkutano na viongozi wakuu wa chama hicho katika hatua ya kutafuta suluhu kuhusu masuala yanayoibua utata.

Tarehe thelathini na moja kamati hiyo itafanya mkutano na wakuu wa TSC. Aidha siku iyo hiyo kutakuwa na mkutano wa pamoja utakaofanyika katika ofisi za wizara hiyo ya leba kujadili mpango wa kuwahamisha walimu, kuwapandisha vyeo na mpango wa kutathimini utendakazi wao.

Waizri huyo amewaomba walimu kuipa kamati hiyo muda wa kufanya mazungumzo kabla ya kuchukua hatua zozote. Kulingana na ratiba ya wizara ya elimu shule zinatarajiwa kufunguliwa kuanzia tarehe tatu Januari.Wiki moja iliyopita Katibu Mkuu wa KNUT Wilson Sossion aliapa kwamba mgomo wao utaanza shule zitakapofunguliwa mwakani kuishinikiza TSC kushughulikia malalamiko yao.

Hayo yanajiri wakati ambapo KNUT imesisitiza kuwa mgomo wa walimu utaendelea jinsi ulivyopangwa. Mweka Hazina wa Kitaifa wa KNUT John Matiangi amesema TSC imekuwa ikipuuza malalamiko ambayo yamekuwa wakiwasilishwa na chama hicho.