array(0) { } Radio Maisha | Wakili, Tom Ojienda amekamatwa kufuatia madai ya ufisadi

Wakili, Tom Ojienda amekamatwa kufuatia madai ya ufisadi

Wakili, Tom Ojienda amekamatwa kufuatia madai ya ufisadi

Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI wamemkamata Wakili Tom Ojineda kwa madai ya kuhusika na ufisadi katika kampuni ya sukari ya Mumias.

Ojienda amekamtwa na kupelekwa katika makao makuu ya DCI kuhojiwa. Aidha washukiwa wengine wa sakata hiyo wanatafutwa.

Huneda wakili huyo akalazimika kusalia korokoroni hadi Jumatatu atakapofikishwa mahakamani. Idhini ya kukamatw akwa Ojienda ilitolewa wiki iliyopita na Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji, baada ya kupokea faili ya uchunguzi wa madai hayo.

Mafaisa wa DCI na wake wa DPP wamekuwa wakichunguza madai ya kuibiwa kwa shilingi milioni 200 kutoka kwa kampuni ya sukari ya Mumias.

Kukamatwa kwa Ojienda kunajiri wakati ambapo mfutano umekuwa ukishughudiwa baina yake na Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA kufuatia madai ya kukwepa kulipia kodi, ya shilingi milioni 3.6.

Hata hivyo Ojienda aameishtaki KRA na kukana madi hayo akisema ni njama ya kutaka kumzuia asiteuliwe kukiwakilisha Chama cha Wanasheria LSK katika Tume ya Huduma za Mahakama JSC.