array(0) { } Radio Maisha | Matiang'i aagiza machifu na manaibu wao Kaprotet, Bomet wachunguzwe

Matiang'i aagiza machifu na manaibu wao Kaprotet, Bomet wachunguzwe

Matiang'i aagiza machifu na manaibu wao Kaprotet, Bomet wachunguzwe

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Fred Matiang'i ameagiza uchunguzi kufanywa dhidi ya machifu na manaibu wao eneo la Kaprotet Kaunti ya Bomet kufuatia utepetevu kazini. Matiang'i ameagiza uchunguzi huo baada ya kupata ripoti kwamba idadi kubwa ya watoto wadogo walilazwa hospitalini baada ya kubugia pombe haramu aina ya chang'aa.

Amemtaka Kamishna wa Kaunti kuwachukulia hatua hiyo iwapo itabainikwa kuwa walizembea kazini.

Wakati uo huo, amerejelea msimamo wa serikali kwamba wataendelea na msako dhidi ya wagemaji wa pombe haramu.