array(0) { } Radio Maisha | IPOA yaanzisha uchunguzi kufuatia kuuliwa kwa mwanafunzi wa chuo kikuu

IPOA yaanzisha uchunguzi kufuatia kuuliwa kwa mwanafunzi wa chuo kikuu

IPOA yaanzisha uchunguzi kufuatia kuuliwa kwa mwanafunzi wa chuo kikuu

Mamlaka ya Kutathimini Utendakazi wa Polisi, IPOA imeanzisha uchunguzi kufuatia kisa ambapo mwanafunzi wa chuo kikuu anadaiwa kuuliwa na maafisa wa polisi mtaani Kibra, Nairobi.  Katika taarifa kwa vyombo vya habari IPOA hata hivyo haijafafanua iwapo wamemtambua afisa wa polisi anayehusishwa na mauaji hayo.

Tayari Shirika la Kutetea Haki za Binadamu, la Amnesty Internation limekashfu vikali maujai hayo huku likimtaka Inspekta mkuu wa polisi kuhakikisha uchunguzi unaharakishwa. Iimekitaja kisa hicho kuwa mojawapo ya mauaji ya kiholela yanayotekelezwa na polisi. Taarifa hii inajiri saa chache tu baada ya Inspekta Mkuu wa Polisi, Joseph Boinnet kuiagiza IPOA kuharakisha uchunguzi huo.

Carlton Maina mwenye umri wa miaka ishirini na mitatu ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Leeda Nchini Uingereza anadaiwa aliuliwa makusudi na maafisa wa polisi tarehe 22 mwezi huu.  Licha ya baadhi ya walioshuhudia kudai kuwa maafisa waliomuua walikuwa na njama fiche.

Polisi wanadai kuwa Maina ni miongoni mwa genge la wahalifu ambalo limekuwa likiwahangaisha wakazi wa Kibera.

Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya visa vya maujai ya kiholea ambavyo vinadaiwa kutekelezwa mwaka huu ni zaidi ya mia nane.