array(0) { } Radio Maisha | NTSA yayapokonya leseni magari 11 ya uchukuzi wa umma

NTSA yayapokonya leseni magari 11 ya uchukuzi wa umma

NTSA yayapokonya leseni magari 11 ya uchukuzi wa umma

Mamlaka ya Usalama Barabarani NTSA imeyapokonya jumla ya magari ya uchukuzi wa umma kumi na moja leseni kwa kukiuka sheria za tarafiki. Magari yaliyopokonywa leseni hayataruhisiwa kuendesha shughuli zozote kwa kipindi cha mwezi mmoja. 

Katika taarifa kwa vyombo vya habari NTSA aidha imesema imewapokonya leseni madereva sita kwa kipindi cha mwaka mmoja na mwingine kwa kipindi cha miaka miwili kwa kukiuka sheria hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Francis Mejja amesema kwamba wamepokea malalamiko kutoka kwa umma kuhusu baadhi ya magari ambayo yameongeza nauli msimu huu wa sherehe, hivyo kukiuka sheria za trafiki. Amesema wamewaarifu maafisa wa trafiki kushirikiana nao kuendeleza msako ili kuwanasa wahudumu zaidi wa magari wanaoiuka sheria.

Kando na hayo Mejja ameyaonya magari yasiyo na leseni ya kuhudumu usiku kukoma kwani yanaweza kuchangia ajali za barabarani msimu huu.