array(0) { } Radio Maisha | Maraga na mkewe wajeruhiwa katika ajali

Maraga na mkewe wajeruhiwa katika ajali

Maraga na mkewe wajeruhiwa katika ajali

Jaji Mkuu, David Maraga na mkewe Yucabeth Nyaboke wanatarajiwa kusafirishwa hadi jijini Nairobi kwa matibabu zaidi kufuatia agizo la Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuhusika ajali ya barabarani. Wawili hao wamehusika ajali eneo la Ngata kwenye Barabara Kuu ya Nakuru-Eldoret na kupelekwa katika Hospitali ya War Memorial kwa matibabu.

Mshirikishi wa Utawala eneo la Bonde la Ufa, Mogo Chimwaga amesema wawili hao walikuwa wakielekea kwa hafla ya kanisa wakati kisa hicho kilipotokea.

Maraga amepata majeraha ya kichwa huku mkewe akipatwa na mshtuko japo hali yao imeimarika.Gari lao liligongwa na jingine la binafsi japo dereva hakujeruhiwa.