array(0) { } Radio Maisha | Taharuki yazidi Njoro kufuatia mapigano

Taharuki yazidi Njoro kufuatia mapigano

Taharuki yazidi Njoro kufuatia mapigano

Taharuki ingali imetanda eneo la Njoro Kuanti ya Nakuru, huku wakazi waliokuwa wakikita kambi katika shule mablimbali eneo hilo wakiagizwa hukama ili kupisha shughuli za masomo kuanzia Jumatatu ijayo. Hata hivyo baadhi yao, wamelalamika kwamba hawana mahali pa kwenda na kuwataka viongozi kuwatafutia makazi mbadala.

Wakati uo huo wawakilishi wadi wa Kaunti ya Nakuru sasa wanataka Naibu Spika Samuel Tonui aliyekamatwa kufuatia ghasia hizo aachiliwe. Wawakilishi wadi hao zaidi ya ishirini na watano wamekita kambi katika kituo cha polisi cha Njoro ambapo Tonui anazuiiliwa wakitaka aachiliwe, hadi pale uchunguzi utakapokamilika. Wakiongozwa na Kiongozi wa wengi Stanley Karanja wamesema kuendelea kuzuiliwa kwa Tonui kutasababisha ghasia zaidi kutokea.

Tonui alikamatwa jana jioni kwa madai kwamba amechochea ghasi maeneo ya Nessuit na Marioshoni.

Hyao yanajiri huku wabunge wawili wamewasilisha ombi kwa Tume ya Uwiano na Utangamano wa Taifa,  NCIC kumchunguza Seneta wa Narok Ledama Ole Kina kufuatia mapigano ambayo yanaendelea kushuhudiwa eneo la Mau.

Nelson Koech  wa Belgut na mwenzake wa Soin-Sigowet, Kipsengeret Koros  Ledama ameonekana akitoa matamshi ambayo huenda yamechochea mapigano hayo.
Mapema leo Polisi wameumuua mtu mmoja eneo la Nessuit, Mau Mashariki aliyewafumania polisi akiwa na wenzake kwa lengo la kuwakabili kwa mishale. Mshirikishi wa utawala eneo hilo, Mwongo Chimwanga alisema kundi la watu waliojihami kwa mishale liliwafumania polisi usiku wa kuamkia leo wakiwa katika harakati za kushika doria hali iliyochangia kuuliwa kwa mmoja wao.