array(0) { } Radio Maisha | Polisi wawakamata watu waliokuwa wakisafirisha samaki waliooza, Eldoret

Polisi wawakamata watu waliokuwa wakisafirisha samaki waliooza, Eldoret

Polisi wawakamata watu waliokuwa wakisafirisha samaki waliooza, Eldoret

Maafisa wa Mamlaka ya Ukadiriaji Ubora wa Bidhaa Nchini KEBS kwa ushirikiano na wale wa Idara ya Uplelezi mjini Eldoret, wanaendelea na uchunguzi kufuatia kunaswa lwa lori moja lililokuwa likisafirisha samaki ambao wanaaminika sio salama kwa matumizi ya binadamu. Dereva na kondaklta wa lori hilo wamezuiliwa huku wakiendelea  kuhojiwa .

Makasha 2,000 ya samaki yalipatikana  ndani ya lori hilo huku ikibainika kuwa baadhi walikuwa tayari wameoza kufuatia muda mrefu wa usafiri licha ya stakabadhi zake kuonesha kuwa walifaa kuuzwa kufikia mwaka wa 2020.

OCPD wa Eldoret Magharibi Zachariah Bitok amesema taarifa walio nayo kwa sasa,ni kwamba makasha hayo yalisafishwa kutoka Uchina kupitia bandari ya Mombasa japo ameshikilia kuwa uchunguzi unafanywa na idara zinazohusika ili kubaini msingi wake.