array(0) { } Radio Maisha | Wanawake wataka Sharon kutendewa haki

Wanawake wataka Sharon kutendewa haki

Wanawake wataka Sharon kutendewa haki

Wito umetolewa kwa maafisa wa usalama kuvitwaa vyeti vya usafiri vya washukiwa wakuu wa mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, Sharon Otieno. Wito huo umetolewa na makundi ya wanawake wa matabaka mbalimbali walioandamana jijini Nairobi leo hii kushinikiza haki kutendeka huku wakihofia kwamba huenda washukiwa wa mauaji ya Sharon wakatoweka nchini iwapo vyeti vyao vya  usafiri havitatwalia. 


Aidha wameiomba serikali kuipa ulinzi familia ya Sharon baada ya siku chache zilizopita mamake kuelezea wasiwasi kuhusu usalama wao huku uchunguzi wa kuwakabili wahusika wa mauaji ukiendelea.

Wakati uo huo wamelalamikia shutma zinazoendelezwa na baadhi ya watu dhidi ya Sharon hasa kutokana na madai kwamba huenda mzozo wa kimapenzi ulichangia mauaji yake wakisema hakuna mtu anayestahili kuuliwa kikatili jinsi alivyofanyiwa mwanafunzi huyo.