array(0) { } Radio Maisha | Osotsi alalamikia sukari inayodaiwa kuwa ya Mumias

Osotsi alalamikia sukari inayodaiwa kuwa ya Mumias

Osotsi alalamikia sukari inayodaiwa kuwa ya Mumias

Huku kitendawili cha iwapo sukari iliyoingizwa nchini ni salama au la, kikingali kuteguliwa, biashara ya bidhaa za magendo bado imenoga nchini huku nembo ya Kiwanda cha Sukari cha Mumias kikitumiwa.

Mbunge maalum, Godfrey Osostsi analalama kwamba licha ya kiwanda hicho kutoendesha shughuli zozote kwa miezi sita, bado kuna sukari yenye nembo ya Mumias katika maduka mbalimbali nchini.

<AUDIO>9665

Amesema sukari ambayo inauzwa madukani kwa sasa haioneshi tarehe ya kutengenezwa wala tarehe ya mwisho wa matumizi.

 

Aidha Osotsi anasema amezungumza na usimamizi wa kiwanda hicho na wamethibitisha kwamba sukari yenye nembo ya Mumias inayouzwa sokoni si bidhaa yao.

Osotsi ametaka serikali kufanya uchunguzi ili kubaini ni akina nani wanauza sukari yenye nembo ya Mumias. Amesema licha ya mchakato wa kufufuliwa tena kwa kiwanda hicho ukiendelea, huenda hasara ikashuhudiwa iwapo walaghai wanaotumia nembo yake hawatatiwa nguvuni na kushtakiwa.

Ikumbukwe bunge lilitupilia mbali ripoti ya sukari bungeni huku kukiibuliwa madai ya rushwa ili kufutilia mbali ripoti hiyo kwa madai kwamba ilikuwa imekarabatiwa kuyaondoa majina ya baadhi ya washukiwa. Aidha baadhi ya wabunge waliibua madai kwamba ripoti hiyo haikujibu madai kuwa sukari iliyoingizwa nchini ina madini hatari au la.