Zarika "Iron Fist "ahifadhi ubingwa wa WBC

Zarika "Iron Fist "ahifadhi ubingwa wa WBC

Mwanandondi Fatuma Zarika amehifadhi ubingwa wake wa dunia wa WBC upande wa akina dada kwenye uzani wa Super Bantam.

Zarika alilazimika kutumia ufundi zaidi kuhifadhi ubingwa huo kwa mara ya pili alipomshinda mwanandondi wa Mexico Yamileth Mercado kwa kuzijizolea alama nyingi  kuliko mpinzani wake kwenye pambano hilo lilo andaliwa kwenye ukumbi wa KICC.

Jaji Eddie Papoe wa Ghana aliweza kumpa Mercado alama 96-94 wakati Majaji Bena Kaloki wa Kenya na Francis Chirwa wa Malawi wakimpa Zarika alama 97-93 na 99-91 mtawalia kwenye pambano hilo la raundi kumi.

Akizungumza baada ya kutawazwa mshindi Zarika amewapongeza wakenya waliyojitokeza kumshangilia akisema ilimpa motisha  wakati wa pigano hilo.

Ushindi wa Zarika unafuatia ule wa Harambee Stars ambao waliwaduwaza Black Stars ya Ghana goli moja kwa bila licha ya kucheza takariban dakika 30 wakiwa wachezaji kumi baada ya beki Philomn Onyango kuoneshwa kadi nyekundu.

Ushindi wa Kenya umefufua matumaini yake ya kufuzu kwa kombe la bara afrika mwaka ujao nchini Cameroun.