array(0) { } Radio Maisha | Rais atakiwa kuwabandua makamishna wa IEBC waliosalia

Rais atakiwa kuwabandua makamishna wa IEBC waliosalia

Rais atakiwa kuwabandua makamishna wa IEBC waliosalia

Viongozi wa dini eneo la Nyanza wametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuwatimua makamishna wote wa Tume ya Uchaguzi, IEBC kwa madai ya kutelekeza majukumu yao na badala yake kufyonza fedha za umma.

Wakiongozwa na Askofu Winnie Owiti, viongozi hao wamesema ilivyo sasa tume hiyo haiwezi kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu tangu kuondoka kwa makamishna wengine hivyo hakuna haja ya kuendelea kuwalipa mishahara minono makamishna waliosalia.

Aidha wamelisihi bunge kuiheshimu katiba na kusitisha mipango ya kubadili tarehe ya uchaguzi kutoka Agosti hadi Disemba. Viongozi hao aidha wameliomba taifa hili kuiga mfano wa taifa la Afrika Kusini kwa kutoa muda wa msamaha kwa watu fisadi na kuwapa fursa ya kurejesha mali ya umma walioitwaa kinyume na sheria.