array(0) { } Radio Maisha | Sonko awakashfu wawakilishi wadi wanaotishia kumbandua

Sonko awakashfu wawakilishi wadi wanaotishia kumbandua

Sonko awakashfu wawakilishi wadi wanaotishia kumbandua

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amewakashfu baadhi ya wawakilishi Wadi wanaotishia kumbandua mamlakani iwapo hatakoma kuendesha majukumu ya Kaunti akiwa nyumbani kwake eneo la Mua, Kaunti Machakos. Sonko amedai vitisho vya wawakilishi wadi hao, vinaingilia maisha yake ya binafsi kwani shughuli za kaunti hazijaathirika.

Gavana Sonko, alianza kuziendeshea shughuli za Kaunti kutoka nyumbani kwake miezi minne iliyopita baada ya kudai kuwa maisha yake yalikuwa hatarini.

Kando na hayo amewataka wawakilishi wadii kukoma kumharakisha kuhusu kumteua Naibu Gavana. Gavana Sonko amesema atafuta ushauri kuhusu suala la kumteua naibu wake kutoka kwa uongozi wa chama cha Jubilee vile vile Mahakama ya Juu.

AidhaSonko amejitenga na madai kuwa alikuwa na ushawishi kwa bunge la Kaunti kumng’atua spika wao Beatrice Elachi akisema bunge lina uhuru wa kumuondoa yeyote.

Ikumbukwe tayari Sonko amewataja Agnes Kagure, Bishop Margaret Wanjiru, Karen Nyamu na Jane Weru, kuwa aliowateua kuchukua wadhfa huo baada Polycap Igathe kujiuzulu.