array(0) { } Radio Maisha | Walimu wafutwa kazi kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi

Walimu wafutwa kazi kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi

Walimu wafutwa kazi kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi

Shule ya upili ya Kitaifa ya Wasichana ya Sironga Kaunti ya Nyamira imekuwa ya hivi punde kukumbwa na madai ya walimu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi.

Tayari madai hayo yamesababisha uhamisho wa walimu wawili wa kiume na wa kike, huku wengine wawili wa kiume kupewa likizo. Inaarifiwa walimu wanne wa shule hiyo wanatuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi.

Aidha walimu wawili ambao wameshukiwa tayari wamepata barua za kuwaachisha kazi kutoka Tume ya Huduma za Walimu, TSC.