array(0) { } Radio Maisha | Mahakama Kuu yasitisha utekelezaji wa kodi ya 16%

Mahakama Kuu yasitisha utekelezaji wa kodi ya 16%

Mahakama Kuu yasitisha utekelezaji wa kodi ya 16%

Mahakama Kuu ya Bungoma imesitisha agizo la Wizara ya Fedha la kutekeleza nyongeza ya kodi ya thamani ya ziada ya asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta hadi kesi iliyowasilishwa na Wakenya watatu wakazi wa Kisumu itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Haya yanajiri huku Waziri wa Fedha, Henry Rotich sasa hivi akiwa katika mkutano na Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi na Kiongozi wa Wengi, Adan Duale kujadili suala hili la nyongeza ya kodi ya thamani ya ziada kwa bidhaa za mafuta.

Siku ya Jumanne Mahakama Kuu ilikataa kusitisha agizo la Waziri Rotich la kuongeza  kodi hiyo. Katika kesi hiyo iliyowasilishwa na Mwananaharakati Okiya Omatata, Jaji Chacha Mwita badala yake aliwataka walioshtakiwa katika kesi hiyo kufika mbele yake ili kujadili jinsi kesi hiyo itasikilizwa na kuitaja hatua hiyo kuwa ni dharura. 

Kwa upande wake Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU umesema utaendelea kushinikiza serikali kusitisha sheria hiyo hadi kilio cha Wakenya wengi kisikike.