array(0) { } Radio Maisha | Spika wa Bunge la Kaunti Beatrice Elachi ajitetea

Spika wa Bunge la Kaunti Beatrice Elachi ajitetea

Spika wa Bunge la Kaunti Beatrice Elachi ajitetea

Spika wa Bunge la Nairobi Beatrice Elachi amejitetea dhidi ya madai ya ufisadi na utumizi mbaya wa ofisi yake yaliyoibuliwa dhidi yake na baadhi ya wawakilishi wadi. Akizungumza mjini Malindi Elachi amesisitiza kwamba amekuwa akitekeleza majukumu yake kulingana na sheria na haelewi ni kwa nini, wawakilishi wadi wanataka kumbandua. Badala yake amewaomba wawakilishi wa pande zote, kujadiliana ili kutafuta mwafaka iwapo kuna masala yanayostahili kushughulikiwa akisema hakuna haja ya kumbandua spika.

Ikumbukwe wawakilishi wadi Kaunti ya Nairobi watafanya kikao maalum huku suala la wanaomtaka kumbandua Spika  Elachi likiwa kipaumbele. Inaarifiwa kwamba wawakilishi wadi 101 miongoni mwa 122 wametia saini hoja ya kumbandua Elachi.

Kundi hilo linawajumuisha wabunge wa pande zote za kisiasa huku baadhi wakiarifu kwamba huenda hoja hiyo imetokana na hatua ya Elachi kuialika Idara ya Uchunguza kupeleleza madai ya ufisadi katika bunge hilo.