array(0) { } Radio Maisha | Waziri Rotich afanya mkutano na Bunge kuhusu kodi ya thamani ya ziada ya asilimia 16

Waziri Rotich afanya mkutano na Bunge kuhusu kodi ya thamani ya ziada ya asilimia 16

Waziri Rotich afanya mkutano na Bunge kuhusu kodi ya thamani ya ziada ya asilimia 16

Mkutano unaendelea baina ya Waziri wa Fedha Henry Rotich, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kihara Kariuki na Naibu Mkuu wa Utumishi wa Umma, Njee Muturi na Bunge kujadili hatua ya kuanza kutekelezwa kwa Kodi ya Thamani ya Ziada, VAT ya asilimia kumi na sita kwa bidhaa za mafuta. Mkutano huu unalenga kutafuta suluhu ya ukosefu wa mafuta ambao umeanza kushuhudiwa kwenye sehemu mbalimbali nchini.

Mkutano huo unamjumuisha Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, Kiongozi wa Wengi katika Bunge hilo, Adan Duale na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Kimani Ichung'wa. Hayo yanajiri huku magari ya maafisa wa utawala yakionekana yakiyasafirisha mafuta kutoka hifadhi iliyoko eneo la Industrial Area. Aidha inaarifiwa wasafirishaji mafuta katika hifadhi hiyo waliokuwa wakigoma na kukizuia usafirishaji mafuta, wamefurushwa kwa nguvu.

Athari za mgomo huo tayari zimeendelea kushughudiwa kwa siku ya pili leo, kufuatia ukosefu wa mafuta katika vituo vingi vya mafuta hasa jijini Nairobi na miji mingine mikuu. Milolongo mirefu ya magari inaendelea kushughudiwa kwenye baadhi ya vituo vilivyo na mafuta.

Hapo jana juhudi za Tume ya Kuthibiti Kawi, ERC ilifutilia mbali leseni za Muungano wa Binafsi wa Usafirishaji Mafuta, KIPEDA kwa madai ya kushiriki mgomo na kuwahangaisha wasafirishaji wengine, hivyo kuathiri uchumi wa taifa.