array(0) { } Radio Maisha | Mwili wa Sharon Otieno kufanyiwa uchunguzi leo

Mwili wa Sharon Otieno kufanyiwa uchunguzi leo

Mwili wa Sharon Otieno kufanyiwa uchunguzi leo

Mwili wa Manafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo uliopatikana katika msitu wa K'Odera baada ya kuuliwa unatarajiwa kufanyiwa uchunguzi leo hii. Uchunguzi huo utafanyika katika Hospitali ya Rachuonyo Level 4 ambapo mwili wenyewe unahifadhiwa.

Hayo yanajiri huku maafisa kumi na sita waliotumwa kutoka Idara ya Upelelezi DCI hapa jijini Niarobi wakiendelea na uchunguzi kuhusu mauaji hayo. Kulingana na Mkurugenzi wa DCI George Kinoti, matokeo ya uchunguzi huo yanatarajiwa kutolewa baada ya siku tatu. Amesema wote waliohusika watajulikana na kukamatwa.

Ikumbukwe viongozi nchini wanaendelea kushinikiza uchunguzi wa haraka kufanywa kuhusu kisa hicho. Kiongozi wa Chama cha  ODM Raila Odinga amezirai idara za uchunguzi kuhakikisha wahusika wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria. Kauli ambayo imesisitizwa na Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Homabay Gladys Wanga na Mbunge Maalum Dennitah Ghati.

Mwili wa Marehemu ulipatikana ukiwa na majeraha ya kisu, hali ambayo Msemaji wa Polisi Eric Kiraithe aliitaja kuwa iliyoashiria kuwa aliuliwa.

Kumbuka, kifo cha Sharon Otieno, uchunguzi unaoendelea, mjadala ulioibuka kadhalik masaibu wanayoyapitia wanahabari katika kazi yao ni miongoni mwa masuala tukayoangazia katika taarifa yetu kuu siku ya leo.