Serikali yafutilia mbali leseni ya Muungano wa usafirishaji mafuta KIPEDA

Serikali yafutilia mbali leseni ya Muungano wa usafirishaji mafuta KIPEDA

Tatizo la ukosefu wa mafuta nchini limechukua mkondo mwingine baada ya Tume ya Kuthibiti Kawi ERC kufutilia mbali leseni za MMuungano wa Binafsi wa Usafirishaji Mfuta KIPEDA kwa madai nya kushiriki mgomo kulalamikia ongezeko la kodi ya thamani ya asilimia kumi na sita ya bidhaa za mafuta. Katika taarifa kwa vyombo vya habari ERC imeulaumu KIPEDA kwa kuwahangaisha wasafirishaji wengine hivyo kuathiri uchumi wa taifa.

Kufutiliwa mbali kwa leseni hiyo kunamaanisha kuwa Muungano wa KIPEDA hautaruhusiwa kuyanunua mafuta kutoka mataifa ya nje wala kuyasambaza nchini.

Wahudumu wa malori ya kusafirisha mafuta wa muungano huo, wamesusia kazi tangu Jumatatu wiki hii wakilalamikia kuanza kutekelezwa kwa kodi hiyo.

Ikumbukwe hapo jana juhudi za Katibu wa Wizara ya Uchukuzi Andrew Kamau kuwataka wasafirishaji mafuta hao kusitisha mgomo na kurejelea biashara alipofanya ziara katika hiadhi ya mafuta ya Industrial Area zilikosa kuzaa matunda. Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinett vilevile aliwoanya wahudumu hao dhidi ya kufanya maandamano akisema watakamatwa.

Hayo yanajiri huku shinikizo zikizidi kutolewa kwa Rais Uhuru Kenyatta kutia saini mswada uliopitishwa na Bunge kusitisha kutekelezwa kwa kodi hiyo kwa miaka miwili.