array(0) { } Radio Maisha | LSK yaitaka serikali kumpa ulinzi Wakili Charles Kanjama

LSK yaitaka serikali kumpa ulinzi Wakili Charles Kanjama

LSK yaitaka serikali kumpa ulinzi Wakili Charles Kanjama

Chama cha Wanasheria, LSK tawi la Nairobi kimeitaka serikali kumpa ulinzi wakili Charles Kanjama pamoja na mashahidi wanaohusika katika kesi ya jaribio la mauaji ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Kaunti ya Garissa, Idriss Mukhtar.

Katika taarifa, LSK imeonya vikali dhidi ya kupuuzwa kwa madai ya wakili Kanjama kupokea vitisho vya kuangamizwa kwa kuiwakilisha familia ya Mukhtar.

Chama hicho kimetishia kuwashtaki waliomtishia Kanjama pamoja na kuandamana kutafuta haki.

Kanjama alikuwa akimwakilisha mwanamme aliyetuhumiwa kumpiga risasi Mukhtar anayesemekana kujinyonga alipokuwa akizuiliwa korokoroni.

Kupigwa risasi kwa Idris kulisababisha kutiwa nguvuni kwa Gavana wa kaunti hiyo, Ali Korane ambapo alihojiwa katika makao makuu ya polisi jijini Nairobi wiki iliyopita.