array(0) { } Radio Maisha | Kamati ya Bunge kuanza kuchunguza sakata ya ufisadi miongoni mwa wabunge

Kamati ya Bunge kuanza kuchunguza sakata ya ufisadi miongoni mwa wabunge

Kamati ya Bunge kuanza kuchunguza sakata ya ufisadi miongoni mwa wabunge

Kamati ya Bunge la Kitaia ya Mamlaka na Haki leo hii itaandaa vikao vyake vya kwanza kuchunguza madai kwamba wabunge walilipwa kuitupilia mbali ripoti iliyochunguza sakata ya sukari.

Mbunge wa Muhoroni,  Onyango K’Oyoo na Mwenzakewa, Kimilili Didmus Barazani miongoni mwa watu walioratibiwa kufika mbele ya kamati hiyo kutoa ushahidii.

Wawili hao waliibua madai kwamba uchunguzi huo ulifanya na kamati ya pamoja ya bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kieni Kanini Kega na Mwenzake wa Mandera Kusini, haikuwa kamilifu ilipowasilishwa bungeni na ililenga kuwalinda watu fulani.

Mwakilishi wa Kike Kuanti ya Wajir, Fatuma Gedi ni miongoni mwa wabunge walioshtumiwa kwa kupokea hongo kutoiidhinisha ripoti hiyo.